VarsityCollege Network

WANAFUNZI 35,364 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya elimu ya juu katika vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini, kwa mwaka wa masomo wa 2010/2011.

Pamoja na kutangaza majina ya waliochaguliwa, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, imewakaribisha wanafunzi wengine ambao hawakubahatika kuchaguliwa katika awamu hii ya kwanza, kuomba upya ili wafikiriwe tena.

Taarifa iliyotolewa jana na tume hiyo, ilisema wanafunzi hao watajiunga kusomea fani mbalimbali.

Katibu Mkuu wa tume hiyo, Profesa Mayunga Nkunya,alisema 22,553 waliochaguliwa kujiunga na vyuo hivyo ni wavulama na wengine 12,811 ni wasichana.

"Wanafunzi walioomba walikuwa 43,756 na waliochaguliwa ni 35,364. Wanafunzi 8,392 ambao ni asilimia 19.18 hawakubahatika kuchaguliwa ama kwa sababu walikosea katika kufanya uchaguzi wa vyuo au hawakuwa na sifa," alisema Profesa Nkunya.

Alisema hata hivyo, tume imetoa fursa nyingine kwa wanafunzi waliokosea kufanya uchaguzi wa vyuo na ambao hawakuchaguliwa katika awamu hii, kuomba tena.

Alisema Chuo Kikuu cha Dodoma, ndicho kinachoongoza kwa kuchukua wanafunzi wengi zaidi baada ya kuwadahili wanafunzi 5,147, kikifuatiwa na Chuo kikuu cha Dar es Salaam, kilichochukua wanafunzi 48,91.

Alisema wanafunzi waliochaguliwa ni wale tu waliotimiza vigezo na masharti yote yaliyoagizwa.

Pia alisema tume yake imeongeza muda kwa wale ambao walichelewa kuomba na wale waliokosea katika uombaji wa awali

Wakati huohuo Elizabeth Suleiman na Pill Hashim wanaripoti kuwa mwenyekiti wa Kampuni ya IPP Media, Reginald Mengi ametoa hundi ya Sh13 milioni kwa wanafunzi 13 wa Shule ya Sekondari Azania ya jiji Dar es Salaam waliofanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha sita na kupata daraja la kwanza.

Mengi alitoa fedha hizo kwa wanafunzi hao, kufuatia ahadi aliyoitoa Februari mwaka huu, wakati akiwa mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha sita katika shule hiyo.

Alisema ni kipindi cha wanafunzi hao kujijenge moyo wa kujiamini na kusoma kwa bidii ili kuweza kutimiza ndoto zao na kufanikiwa katika maisha.

Mwananchi

Views: 1402

Comment

You need to be a member of VarsityCollege Network to add comments!

Join VarsityCollege Network

¬© 2016   Created by Abbas Kitogo.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service